Afisa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Risala Kabongo akimvisha skafu Kiongozi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Helen Clark baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Mkuu wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Hellen Clark amesema kuwa shirika hilo litaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania kupambana na ujangili na kuhifadhi maliasili kwa ajili ya matumizi ya sasa na baadaye. (HM)
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Mradi Mradi kuimarisha mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST) unaofadhiliwa na shirika hilo, Clark alisema misaada hiyo italenda kuimarisha utendaji kazi wa watumishi katika kukabiliana na ujangili.
Alisema mapambano dhidi ya ujangili yanahitaji mkakati wa pamoja kati ya Mashirika ya misaada, jamii, serikali na Mamlaka husika na kuwa rasilimali zilizopo zinahitajika kulindwa kwa ajili ya matumizi ya vizazi vilivyopo na vijavyo hivyo inahitajika jitihada za makusudi kwa wadau wote wa maendeleo ndani ya nje ya nchi.
Clark alisema ametembea katika hifadhi hiyo na kuweza kujionea shughuli zinazofanywa na SPANEST hasa katika kuboresha utalii nyanda za juu kusini ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa askari na watumishi wengine, kuboresha mawasialiano kwa kutoa vifaa na mitambo.
Paul Harrison ambaye ni Mshauri wa wanyama wa UNDP alisema lengo la mradi huo ni kuboresha matumizi ya rasilimali na kukuza utalii katika eneo la nyanda za juu kusini kwa kuimalisha mifumo ya ulinzi, miundo mbinu na mawasiliano kwa watumishi wa hifadhi.
Alisema pia serikali inatakiwa kuwa na mkakati thabiti na kuchangia katika kuboresha utendaji wa watumishi ikiwemo kuwapatia malipo mazuri, vitendea kazi na mafunzo jambo litakalosaidia kupunguza vitendo vya ujangili kwa kiasi kikubwa.
Alisema eneo la ikolojia ya Ruaha ndilo lenye tembo wengi kwa sasa na inatakiwa wadau wa utalii waone kuwa tembo ni zaidi ya mnyama kwa kuwa anaweza kuboresha uchumi wao na Taifa.
Harrison alisema kinachofanyika ni kuwasiliana na wadau mbalimbali wa kimataifa na kusisitiza kutonunua bidhaa zitokanazo na meno ya tembo ili kusaidia kupunguza vitendo vya ujangili.
Naye Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi alisema UNDP na mashirika mengine ya kimataifa yamekuwa msaada mkubwa katika mapambano dhidi ya ujangili na kuwa TANAPA wanathamini mchango huo.
Hivi karibuni UNDP kupitia mradi wa SPANEST ilitoa msaada wa Greda na magari matatu vyenye thamani ya zaidi ya Sh1.2 Bilioni, greda zaidi ya Sh570m na Land Cruser Pick Up Sh540m na kuwa gari moja litolewa kwa ajili ya hifadhi ya kitulo na mawili Ruaha