Emiliana Fidelis akiwa amesimama mbele ya meza ya majaji mara baada ya majaji kufurahishwa na kuvutiwa na Kipaji chake, Emiliana ni mmoja kati ya waliotakiwa kuwa mshindi wa Kanda ya ziwa ila kwa bahati mbaya Umri wake ndio ulikuwa kikwazo.
Jaji Yvonne Cherry akimkabidhi zawadi ya shilingi laki Moja Mshiriki Emiliana Fidelis mara baada ya kuvutiwa na Kipaji chake huku akiwa mshiriki pekee mwenye umri mdogo kuliko wote kwenye mashindano ya Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents.
Hawa ndio washiriki walioingia tano bora
Mshiriki Crensenciah Herman akilia kwa furaha mara baada ya Kutajwa kuwa mmoja kati ya washindi katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lilomalizika Leo Mkoani Mwanza
Jaji Mkuu wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania
yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents, Roy Sarungi akimkabidhi zawadi
mmoja wa Washindi watatu wa mashindano hayo mara baada ya kutangazwa
washindi.
Jaji Single Mtambalike akimpongeza mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuibuka kidedea katika Mashindano ya Tanzania Movie Talents.
Majaji wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi watatu wa Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza mara baada ya Kuwatangaza na kuwakabidhi washindi zawadi zao.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza